Ufunuo wa Yohana 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 6 (Swahili) Revelation 6 (English)

Kisha nikaona napo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! Ufunuo wa Yohana 6:1

I saw that the Lamb opened one of the seven seals, and I heard one of the four living creatures saying, as with a voice of thunder, "Come and see!"

Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda. Ufunuo wa Yohana 6:2

And behold, a white horse, and he who sat on it had a bow. A crown was given to him, and he came forth conquering, and to conquer.

Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo! Ufunuo wa Yohana 6:3

When he opened the second seal, I heard the second living creature saying, "Come!"

Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa. Ufunuo wa Yohana 6:4

Another came forth, a red horse. To him who sat on it was given power to take peace from the earth, and that they should kill one another. There was given to him a great sword.

Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Ufunuo wa Yohana 6:5

When he opened the third seal, I heard the third living creature saying, "Come and see!" And behold, a black horse, and he who sat on it had a balance in his hand.

Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai. Ufunuo wa Yohana 6:6

I heard a voice in the midst of the four living creatures saying, "A choenix{A choenix is a dry volume measure that is a little more than a litre (a little more than a quart).} of wheat for a denarius, and three choenix of barley for a denarius! Don't damage the oil and the wine!"

Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! Ufunuo wa Yohana 6:7

When he opened the fourth seal, I heard the fourth living creature saying, "Come and see!"

Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi. Ufunuo wa Yohana 6:8

And behold, a pale horse, and he who sat on it, his name was Death. Hades followed with him. Authority over one fourth of the earth, to kill with the sword, with famine, with death, and by the wild animals of the earth was given to him.

Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Ufunuo wa Yohana 6:9

When he opened the fifth seal, I saw underneath the altar the souls of those who had been killed for the Word of God, and for the testimony of the Lamb which they had.

Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Ufunuo wa Yohana 6:10

They cried with a loud voice, saying, "How long, Master, the holy and true, until you judge and avenge our blood on those who dwell on the earth?"

Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao. Ufunuo wa Yohana 6:11

A long white robe was given to each of them. They were told that they should rest yet for a while, until their fellow servants and their brothers,{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} who would also be killed even as they were, should complete their course.

Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, Ufunuo wa Yohana 6:12

I saw when he opened the sixth seal, and there was a great earthquake. The sun became black as sackcloth made of hair, and the whole moon became as blood.

na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Ufunuo wa Yohana 6:13

The stars of the sky fell to the earth, like a fig tree dropping its unripe figs when it is shaken by a great wind.

Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Ufunuo wa Yohana 6:14

The sky was removed like a scroll when it is rolled up. Every mountain and island were moved out of their places.

Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, Ufunuo wa Yohana 6:15

The kings of the earth, the princes, the commanding officers, the rich, the strong, and every slave and free person, hid themselves in the caves and in the rocks of the mountains.

wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Ufunuo wa Yohana 6:16

They told the mountains and the rocks, "Fall on us, and hide us from the face of him who sits on the throne, and from the wrath of the Lamb,

Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?

Ufunuo wa Yohana 6:17

for the great day of his wrath has come; and who is able to stand?"